Yanga na Mtibwa Sugar zinapambana kesho (Februari 2 mwaka
huu) katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam .
Mwamuzi Ronald Swai kutoka Arusha ndiye atakayechezesha
mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani wakati Yanga ikiongoza
ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mechi iliyopita walilala mbele ya
Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo wa ligi kwa sasa.
Polisi Morogoro itakuwa mwenyeji wa African Lyon kwenye
Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro wakati Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga
utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ruvu Shooting
inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa.
Keshokutwa (Jumapili) kutakuwa na mechi mbili. Simba
itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Tanzania Prisons
ikiikabili Coastal Union katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Comments
Post a Comment