WAMBURA KUZUIA UCHAGUZI TFF MAHAKAMANI IWAPO.....



ALIYEKUWA katibu mkuu FAT (sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Michael Wambura, kwa mara nyingine amekusudia kwenda mahakamani iwapo uongozi wa TFF utafanya uchjaguzi wa viongozi kwa kutumia kanuni mpya.
 Wambura amesema leo kwamba amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kufanyika kwa njama ili uchaguzi usifanyike ama uharibike na viongozi waliopo sasa waendelee kuwepo madarakani.
Alisema katiba iliyotumika kuitisha uchaguzi huo ni batili kwa kuwa mabadiliko yake hayakufuata utaratibu wa kikatiba kwani hakuna mkutano mkuu wowote wa TFF uliokaa kupitisha mabadiliko hayo.
“TFF imempotosha msajili wa vyama kupitia ibara ya 76 ya katiba ya TFF ya kuwa Mkutano mkuu wa TFF ulikutana Desemba 15, 2012 kufanya mabadiliko hayo huku ikijua sio kweli, ninapenda kuitahadharisha TFF hili sio suala mchezo ni swala la kisheria, hibyo kwa mujibu wa sheria za nchi mwenye mamlaka ya kutafsiri sheria (katiba) ni mahakama hivyo ushauri wangu kwa TFF ili kuondoa uwezekano wa mkono wa sheria kuingia hawana budi kufuata haya,’alisema
Mosi, Wambura ametoa pendekezo la kusimamisha matumizi ya katiba hiyo mara moja kwani sio halali kuondoa uwezekano wa kutafutwa haki kwenye mahakama za kiraia.
Pili Wambura ameitaka TFF kuyafuta maamuzi yote na kuivunja kamati ya rufaa ya uchaguzi inayoongozwa na Iddi Mtinginjola an ili matakwa ya kikatiba ya uchaguzi yatimie rufani zote zirudishwe kwenye kamati ya rufaa kama katiba halali inavyotaka ili kukamilisha mchakato wa uchaguzi.
Tatu, maamuzi yakliyofanywa na kamati ya uchaguzi chini ya Lyato (Deo-Mwenyekiti wa kamati) yaheshimiwe na kama kuna wasioridhika wakate rufgaa kamati ya rufaa ya TFF, pamoja na kuwa maamuzi ya Lyatto hayana maamuzi ya moja kwa moja nay eye lakini ataweka misingi bora ya kikatiba.
Akifafanua zaidi, Wambura alisema kwa mujibu wa katiba mpya ambayo yeye anaiita sio halali ibara ya 76 katiba hiyo imeanza kutumika desemba 15,2012 na kanuni za uchaguzi zimeanza kutumika januari 7, 2013 ambapo kanuni hizo na katiba yake ndio zilizotumika kuitisha uchaguzi mkuu.
“Baada ya kupitisha katiba mpya na kuanza kutumika TFF ilipaswa kuunda kamati mpya ya uchaguzi, kwa mujibu wa katiba ya TFF ibara ya 49 (4) mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi anapaswa kuwa na taaluma ya sheria sifa ambayo Lyatto hana  na hivyo ushiriki wake kuwa kinyume na katiba ya TFF, hali ianyoufanya uchaguzi wake kuwa batili na unapaswa kufutwa na kuteua kamati mpya ili mchakato uanze upya hivyo kuchelewesha kupatikana kwa viongozi wapya wa TFF,”alisema
“Kanuniu hutengenezwa ili kuwezesha utekelezaji wa katiba husika hivyo katiba hupitishwa na kusajiliwa kwanza na baadaye hutungwa kanuni, cha kushangaza kanuni za uchaguzi za TFF zilipitishwa na kusainiwa na Januari 7, 2013  wakati katiba ya TFF ilisajiliwa na kugongwa muhuri wa msajili Januaro 10 siku tatu baada ya kanuni kusasiniwa.
“Swala linakuja kanuni hizi zilitungwa kwa mujibu wa katiba batili kisheria, ninaishauri TFF ili kuondoa uwezekano wa kuingiza TFF kwenye mgogoro wa kisheria, uamuzi wa busara wa kuachana na katiba batili ni muhimu kwa maendeleo ya soka Tanzania kwa kusimamisha matumizi ya katiba mpya batili ya TFF na matokeo ya maamuzi yote yanatokana na katiba hiyo,”alisema
Awali, Wambura ambaye alikuwa akigombea nafasi ya makamu wa Rais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika februari 24, jina lake lilienguliwa kutokana na sababu kadhaa ikiwemo suala la uadilifu.
Alisema matarajio yake ya kuwania nafasi hiyo yalianza kuingia dosari kwa mara ya nne  tangu 2008 katika chaguyzi mbalimbali ambazo TFF ina maslahi nazo ambapo jina klake liliondolewa na kamati ya uchaguzi kwa sababu mbalimbali.


Comments