Mechi namba 121 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi
(Februari 24 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Mtibwa Sugar
kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba imeingiza sh. 239,686,000.
Watazamaji 10,669 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo
ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku
kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,577,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,467,694.92.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi
ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 9,491 na kuingiza sh. 47,455,000 wakati
idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia
washabiki 105 na kuingiza sh. 2,100,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh.
7,412,162.26, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,447,297.36, Kamati
ya Ligi sh. 4,447,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,223,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,729,504.53.
Comments
Post a Comment