OMMY DIMPOZ KUPAMBA REDD'S MISS TABORA 2013

MSANII OMMY DIMPOZI KUTUA MISS REDDS TABORA 2013/14
Sarahy Paul mshindi wa mwaka jana 2012

Mashindano ya Miss Redds Tabora kukujia tena kwa sura pevu zaidi, hii ni baada ya kufanyika mashindano kama haya mwaka jana na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, sasa ni zamu nyingine yaliyonuwiwa kuwa na ubunifu wa kutosha kwa maandalizi kabambe yaliyofanywa tayari kuanzia sasa.
Nikiwasiliana kutoka SPAIN BARCELONA na muandaaji wa mashindano haya kwa miaka minne (4) sasa mfululizo toka akabidhiwe kutoka kwa muandaaji wa zamani Mbunge wa sasa mjini Tabora Mh. Rage chini ya V.O.T FM Mgalula Fundikira ambaye kwasasa ni wakala aliyepewa tena idhini ya kuyaandaa shindano hili kutoka kwa LINO INTERNATIONAL wenye hati na idhini ya kuandaa mashindano haya toka ngazi za vitongoji hadi mashindano makubwa ya MISS TANZANIA.

"....uwakala wangu unaendelea baada ya kuombwa na 
LINO INTERNATIONAL kuandaa tena mwaka
 huu na  sasa hivi na msanii Ommy Dimpoz na msanii atakaye mchagua yeye Dimpoz watakuwepo kutoa burudani ya kutosha..." 
Alisema Mgalula akiwa Spain Barcelona.
*************
Kuhusu form za ushiriki zitatangazwa mapema wiki ijayo wapi zitapatikana na taratibu zote za mashindano utapata kuzifahamu vizuri.
TIMIZA NDOTO ZAKO ZA KUIBUKA MREMBO WA MISS REDDS TABORA.

Nani ungependa awe msanii atakaye chaguliwa na Ommy D?

Habari Na http://www.aloyson.com/