NIYONZIMA AYEYUSHA KONI ZA AZAM

KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima 'Fabregas'  amezidi kuiimarisha timu yake katika kilelele cha ligi kuu bara baada ya kuifungia bao la ushindi timu yake dhindi ya Azam Fc katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa.
Licha ya Azam kuonekana na uchu mkubwa wa kutaka kuendeleza ubabe wao kwa Yanga kama walivyofanya kwenye mzunguko wa kwanza, walishindwa kufua dafu baada ya kukutana na ukuta madhubuti wa Yanga.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 39 huku Azam Fc ikibaki na pointi zake 36 na kuendelea kushika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.