MILOVAN:SIONDOKI BONGO MPAKA SIMBA MNILILIPE CHANGUALIYEKUWA kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic amesisitiza kutoondoka nchini mpaka uongozi utakapomlipa fedha zake kiasi cha dola 32,000.
Milovan ambaye alitupiwa virago na uongozi mwaka jana baada ya kushinda kuipatia mafanikio timu hiyo, aliwasili nchini wiki iliyopita kwa ajili ya kufuatilia fedha zake hizo, huku uongozi ukidai utamlipa baada ya kupokea fedha za mauzo ya mshambuliaji wake Emmanuel Okwi kutoka klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Milovan amesema  kwamba itamuwia vigumu kwenda kwao na baadaye kurudi tena ncvhini kwa ajili ya kufuatilia fedha zake kwani gharama za usafiri ni kubwa sana.
Akizungumzia suala hilo, Kamwaga alisema watamlipa fedha zake kocha huyo lakini si za Okwi kwani hizo zitatumika kwa matumizi yaliyopangwa tangu awali.
Kamwaga alisema kwamba wanashangazwa na Milovan kuja nchini bila taarifa yoyote wakati walikubaliana kuwa watamtumia fedha zake kwa kumuwekea kwenye akaunti yake.