PAMBANO la Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Libolo
FC ya Angola
lililofanyika jana (Februari 17 mwaka huu) limeingiza sh. 133,795,000 wakati
lile la Kombe la Shirikisho kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini
lililochezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) limeingiza sh. 34,046,000.
Watazamaji 22,469 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Simba
kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Simba ilipoteza pambano hilo
kwa bao 1-0.
Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za
waamuzi sh. 24,926,500, gharama za tiketi sh. 7,410,000, asilimia 15 ya uwanja
baada ya kuondoa gharama za waamuzi na tiketi ilikuwa sh. 15,218,775, asilimia
10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) sh. 10,145,850 na asilimia 75 iliyokwenda klabu ya Simba ni
sh. 76,093,875.
Mechi ya Azam iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi
wa mabao 3-1 ilishuhudiwa na watazamaji 13,431 kwa viingilio vya sh. 2,000, sh.
5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000. Mgawo katika mechi hiyo ulikuwa kama ifuatavyo;
Gharama za tiketi sh. 4,779,000, asilimia 15 ya uwanja baada
ya kuondoa gharama za tiketi ilikuwa sh. 4,390,050, asilimia 10 ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 2,926,700 na asilimia 75 iliyokwenda Prime Time Promotions (Azam) ni sh.
29,267,00.
Comments
Post a Comment