BOBAN, NGASSA WATUA ASRUSHA KUONGEZA NGUVU

VIUNGO wa Simba, Mrisho Ngasa na Haruna Moshi 'Boban' wameungana na wenzao jijini Arusha tayari kwa mchezo wao wa ligi kuu bara dhidi ya maafande wa JKT Oljoro utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo.
Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema nyota hao hawakuambatana na wenzao jana kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya mambo, hivyo uwepo wao Arusha utaongeza hamasa zaidi ya mchezo wa kesho.
Amesema kikosi cha Simba kipo vizuri na tayari kwa mchezo wa kesho.