WACHEZAJI YANGA WAWA GUMZO UTURUKI


WACHEZAJI wa klabu ya Yanga wamekuwa gumzo nchini Uturuki kutokana na kuonesha kiwango cha hali ya juu katika mazoezi na michezo yake ya kujipima nguvu. 
Yanga ambayo imepiga kambi ya maandalizi nchini Uturuki imekuwa ikirteka mashabiki wa soka huko ambao hufika kuishuhudia uwanjani. 
Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Binkleb alisema baadhi ya wadau hao wamevutika na viwango vya wachezaji wa timu hiyo kiasi cha kutaka kufahamu zaidi taarifa zao. 
“Kwa kweli kocha na viongozi waliopo huko wanatuambia  kuwa watu wanawafuata sana kuomba kujua wasifu wa wachezaji kwani wanafurahishwa mno na viwango vyao,”alisema. 
Hata hivyo, Binkleb alisema mpaka sasa hakuana wakala ama timu yoyote ya huko ambayo imeonesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji wa timu hiyo. 
Yanga ambayo ipo huko kujiandaa na michuano mbalimbali ikiwemo klabu bingwa Afria Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’ ambao ni mabingwa watetezi pamoja na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom. 
Yanga ikiwa huko imeshacheza mechi mbili ikiwemo dhidi ya Arminia Biefeld ya Ujerumani na kutoka sare ya bao 1-1 kabla ya kutandikwa mabao 2-1 na Denizlispor Fc ya Uturuki mchezo  uliopigwa katika dimba la Selen Football-Kamelya Complex,nchini humo, jioni ya leo itashuka dimbani kukipiga na Emmen Fc inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi. 
Kikosi cha Yanga kinachonolewa na kocha Ernie Brandts kimepiga kambi kwenye hoteli ya hoteli ya Fame Residence Football ambapo pia wanafanya mazoezi.