SIMBA SC WATUA LEO NA MAUJUZI YA UMANGANI


Simba inarejea leo jioni kutoka Oman ilipokwenda kupiga kambi maalum ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom unaotarajiwa kuanza jumamosi ya keshokutwa.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba kikosi hicho baada ya kuwaisili kitaingia  kambini moja kwa moja kujiandaa na  ligi hiyo na michuano ya kimataifa.
Aidha, Simba ambayo itauanza mzunguko huo kwa kucheza na  African Lyon  katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho itaikabili Black Leopards ya Afrika Kusini katika uwanja wa Taifa.