SIMBA SC WASAKA VIDEO ZA LIBOLO


                                          Kikosi cha Simba
UONGOZI  wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, Simba Sc  umepiga hodi ubalozi wa Tanzania nchini Angola kwa ajili ya kusaka video za wapinzani wao kwenye ligi ya mabingwa Afrika. 
Simba imbayo ilikuwa Oman kwa kambi maalum ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakoanza Januari 26, pamoja na ligi ya mabingwa Afrika ambapo itaanza kwa kuivaa Recretivo de Libolo ya Angola kati ya Februari 17 na 19 jijini Dar es Salaam. 
Makamu Mwenyekiti wa Simba alisema kwamba kocha mkuu wa timu hiyo Patrick Liewig ametaka mikanda ya Video za mechi za wapinzani wao hao ili kuweza kuifanyia kazi kabla ya kukwaana nao. 
“Unajua wapinzani wetu hatuwafahamu vizuri hivyo tumeona ni vizuri kusaka mikanda yao ili kuweza kuifanyia kazi kabla ya kukutana nao na tayari tumeshauomba ubalozi wetu nchini Angola utusaidie kwa hili,”alisema 
Kuhusiana na kambi ya timu hiyo, alisema imekuwa na mafanikio makubwa na kocha ameridhishwa na kiwango walichofikia wachezaji wake baada ya kukaa  pamoja kwa wiki mbili sambamba na michezo mitatu ya kujipima nguvu na timu za huko. 
“Kocha ameridhika na wachezaji kuanza kuelewani, hivyo anaamini kwa kiasi kikubwa ametimiza malengo yake aliyojiwekea katika kuhakikisha anaijenga timu tayari kwa mashindano yoyote,”alisema 
Kaburu aliongeza kuwa, timu hiyo itafanya mazoezi ya mwisho leo kabla ya kesho asubuhi kuondoka huko na itakapowasili nchini itaingia kambini moja kwa moja kuendelea na maandalizi yake, kabla ya alhamis kuivaa Black Leopards ya Afrika Kusini kwenye Uwan jaw a Taifa. 
Ikiwa Oman Simba ilicheza mechi tatu za kujipima uwezo ambapo ilianza kwa kukwaana na timu ya Vijana wenye umri chini ya miaka 23 na kufungwa bao 1-0, kabla ya kufungwa 3-2 na Qaboos  na juzi ikaitandika Ahili Sidabi mabao 2-1.

Comments