SIMBA SC KUREJEA J'5, KUIVAA BLACK LEOPARDS ALHAMIS

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba Sc, watarejea nchini keshokutwa kutoka Oman walipokwenda kwa kambi maalum ya wiki mbili.
Simba ilikwenda huko kwa ajili ya kujiandaa na Mzunguko wa pili wa Ligi hiyo pamoja na klabu bingwa ya Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' ameiambia Sports Lady leo kwamba, kikosi cha Simba kesho kitafanya mazoezi yake ya mwisho asubuhi na jioni.
Alisema, Alhamis kikosi hicho kitashuka kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kuikabili Black Leopards ya Afrika Kusini.
Ikiwa Oman simba imecheza mechi tatu za kirafiki ambapo imefungwa mechi mbili na kushinda moja.