ETOILE WAMLIPA OKWI MIL.25 KWA MWEZI

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi atakuwa akipokea dola 17,000 (zaidi ya mil 25 za Tanzania)  kama mshahara wake wa kila mwezi katika klabu yake mpya ya Etoile Du Sahel ya Misri.
Okwi ambaye mapema wiki hii klabu ya Simba ilitangaza kumuuza kwa dola 300,000, mshahara wake huo ni mara nane zaidi ya ule ambao anmgeupata Simba baada ya kuongeza mkataba mpya mwezi Desemba mwaka jana ambao ni dola 3,000 kwa mwezi.