Wachezaji wa Stars
Mwamuzi Sylvester Kirwa kutoka Kenya
ndiye atakayechezesha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Taifa Stars na
mabingwa wa Afrika , Zambia
(Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Kirwa anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) atasaidiwa na Elias Wamalwa na Marwa Range .
Waamuzi hao wasaidizi ambao vilevile watatoka Kenya pia wanatambuliwa na FIFA.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
tayari iko kambini hoteli ya Tansoma, na inafanya mazoezi katika Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume na ule wa Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo
inayotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.
Comments
Post a Comment