STARS,ZANZIBAR HEROES KUSAKA NAFASI YA TATU, CHALENJI


TIMU ya Taifa ya Bara 'Kilimanjaro Stars' na ile ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' sasa zitakutana katika mechi ya kusaka nafasi ya tatu katika michuano ya kombe la Chalenji inayofikia tamati kesho nchini Uganda.
Timu hizo zitakutana katika mchezo huo kesho baada ya jana kufungwa katika michezo yake ya nusu fainali ambapo Heroes ilitolewa kwa matuta na Kenya baada dakika 120 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, huku Stars ikitandikwa na Uganda mabao 3-0.
Kwa matinki hiyo, wenyeji na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Uganda watakwaana na Kenya katika mchezo wa fainali