SIMBA YAMZIBIA NGASSA TFF


WAKATI klabu ya Simba ikiilaani Azam Fc kwa kumuuza mshambuliaji wao Mrisho Ngassa kwa klabu ya El Mereikh ya Sudan, uongozi wa Simba umeishitaki Azam kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF). 
Aidha Simbna imeiomba TFF kutotoa hati ya uhamisho wa kimtaifa ya Ngassa mpaka suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Azam Fc juzi ilitangaza kumuuza Ngassa El Mereikh kwa dau la dola 75,000  huku pia ikitaraji kumlipa dola 50,000 kama dau la kusaini mkataba wa miaka miwili. 
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba, Azam wamefanya uhuni katika kumuuza Ngassa kutokana na ukweli kwamba nyota huyo ana mkataba na Simba ambao utamalizika Mei 31, 2013.
 Alisema kuwa makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wa Ngassa ni kwamba,Simba na Azam zote zina mamlaka na mchezaji huyo hivyo hakuna  timu yoyote itakayofanya maamuzi bila kuishirikisha nyenzake.
 “Pia mkumbuke pia pamoja na dau la dola 25, 000 tulilomchulia Azam Fc, Simba iliingia gharama nyingine za kumshawishi zaidi kama gari, donge nono n.k, pia tulimpa kazi maalum kocha wetu ya kuhakikisha anapandisha kiwango chake,”alisema.