SIMBA SC WAANZA KUNOLEWA NA JULIO

Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom, Simba Sc wameanza mazoezi ya ufukweni chini ya kocha, Jamhuri Kihwelo 'Julio'
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba, Julio atakinoa kikosi hicho kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa ligi hiyo, huku wakisubiri ujio wa kocha wao mpya, Mfaransa,Patrick Liewang anayetarajiwa kutua nchini Desemba 27.
Amsema wachezaji walioanza mazoezi ni wale wasio kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kipo kambini kujiandaa na mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zambia 'Chipolopolo' utakaopigwa Desemba 22 kwenye dimba la Taifa.
"Pia wachezaji ambao hawapo ni wale wa kigeni ambao wapo makwao,"alisema.