NYOTA 27 YANGA SC KUKWEA PIPA LA UTURUKI USIKU WA JUMAMOSI


KIKOSI cha wachezaji 27 wa Yanga Sc kinatarajiwa kuondoka nchini usiku wa jumamosi kuelekea nchini uturuki kwa ajili ya kuweka kambi maalum ya kujiandaa na mashindano mbalimbali.
Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Binkleb ameiambia Sports Lady  maandalizi ya safari hiyo yamekamilika na kwamba wachezaji watakaokwenda huko pamoja na viongozi watajulikana kesho.
Amesema kwamba kambi hiyo itakisaidia sana kikosi katika maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom pamoja na michuano ya Kagame itakayofanyika Kigali, Rwanda ambapo Yanga ni bingwa tetezi.
"Ndo maana tumetaka kwenda Uturuki kwani huko kuna facilities nzuri kwa ajili ya kambi...pia huko tunataraji kiucheza mechi kadhaa za kirafiki,"amesema.

Yanga inayonolewa na Ernie Brandts jana ilichapwa bao 1-0 na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker Fc katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.