MIYEYUSHO AMUADHIBU NASSIB RAMADHAN NA KUTETEA TAJI

 
Bondia Francis Miyeyusho akiwa amebebwa na mashabiki wake kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam usiku huu baada ya kutetea mataji yake ya kimataifa kwa kumpiga Nassib Ramadhan kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya 10.  

Na Mahmoud Zubeiry
BONDIA Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ amefanikiwa kutetea taji lake la WBF uzito wa Bantam, baada ya kumpiga Nassib Ramadhan kwa Techinical Knockout (TKO) raundi ya 10 kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Temeke mjini Dar es Salaam usiku huu.
Nassib alionekana kuishiwa pumzi tangu raundi ya nane, lakini alijikongoja kutaka kumaliza raundi 12 za pambano hilo, ila kwa bahati mbaya, safari ikaishia raundi ya 10.
Hata hivyo, Nassib bondia kutoka Mabibo, Dar es Salaam, alilianza vizuri pambano hilo akimsukumia mpinzani wake makonde mazito yaliyoonekana kumyumbisha.
Naasib aliendelea kutawala pambano hadi raundi ya sita, ila baada ya hapo, mwelekeo wa pambano ulianza kubadilika taratibu, Chichi, Mtoto wa Kinondoni akianza kumuadhibu mpinzani wake kwa makonde yake yaliyoshiba uzito.
Nassib alijitahidi mara moja moja kujibu, lakini zaidi alitumia ujanja wa kumkumbatia Chichi ili kumpunguza kasi.
Hata hivyo, Nassib hakushindwa kwa kupigwa ngumi, bali aliishiwa pumzi jambo ambalo linaashiria kijana huyo ni bondia imara na anaweza kuwa mpinzani wa kweli wa Chichi Mawe.
Kwa ujumla lilikuwa pambano zuri ambalo kwa muda mrefu halijapatikana katika ardhi ya Tanzania- mabondia walikuwa wakipigana, hakukuwa na ujanja ujanja. Wote ni mafundi na mamia waliohudhuria pambano hilo, waliburudika kwa mchezo mzuri.
Katika mapambano ya awali, Deo Samuel alitoka sare na Freddy Sayuni, Mohamed Matumla alimpiga kwa Knockout (KO) raundi ya pili Deo Miyeyusho, Fadhil Majiha alimpiga kwa pointi Juma Fundi na Ibrahim Classic alimpiga kwa pointi Said Mbugi.
Mgeni rasmi, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alimvalisha mkanda wa ubingwa Miyeyusho baada ya pambano hilo, lililohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.  
Mbwana Matumla katikati akiwa George Njavike kulia na King Kiboya kushoto

Hassan matumla na mkewe

Promota Mohamed Bawaziri akiwa Mh, Dk Fenlela

Jamaa alizima mapemaaa, hajaangalia pambano sasa sijui atasimulia nini kitaa

Ibrahim Classic kushoto akimuadhibu Said Mbugi

Bondia mstaafu, Koba Kimanga akizungumza na Thomas Mashali

Msafiri Mgoyi wa TFF akiwa na Yassin Ustadh 

Mabondia wastaafu, Emmanuel Mlundwa na Habib Kinyogoli

Mohamed Matumla akimuadhibu Deo Miyeyusho

Mohamed Matumla akimuadhibu Deo Miyeyusho

Mohamed Matumla akiwa amebebwa juu baada ya kushinda kwa KO raundi ya pili

Juma Fundi kulia akimtupia konde Fadhil Majiha

Jaji akifuatilia kwa makini pambano

Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto kulia akiwa na Dk Fenella meza kuu

Kutoka kulia Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu', Mzee Matumla na Benny Kisaka

Nassib akimtupia konde Francis Miyeyusho

Nassib na Miyeyusho

Nassib na Miyeyusho

Nassib na Miyeyusho

Miyeyusho akimsukumi kitu Nassib

Nassib na Miyeyusho

Konde la Miyeyusho limetua kwenye uso wa Nassib

Nassib na Miyeyusho

Nassib na Miyeyusho

Full maufundi, Nassib na Miyeyusho

Nassib na Miyeyusho

Nassib na Miyeyusho

King Miyeysho ukipenda muite Chichi Mawe

Nassib akiwa amebebwa kutolewa ulingoni

Dk Fenell akimvalisha mkanda Miyeyusho, kushoto ni Mohamed Bawaziri