Mdau Benny Kisaka ambaye ametwaa nafasi ya uwakilishi wa Vilabu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza
uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi
(Desemba 12 mwaka huu) hoteli ya Mbezi
Garden .
Ushindi aliopata Almasi Kasongo aliyechaguliwa kuwa
Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi
ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa DRFA walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya
Utendaji ya DRFA ambayo hivi sasa ina kinara mpya, na kwamba ina changamoto
kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za DRFA kwa kuzingatia katiba na
kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya DRFA chini ya
Juma Simba na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa
kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia katiba na
Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Kasongo
(Mwenyekiti), Meba Ramadhan (Makamu Mwenyekiti), Msanifu Kondo (Katibu), Muhsin
Said (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF), Benny Kisaka (Mwakilishi wa Klabu),
Ally Hobe (Mhazini) na wajumbe Mohamed Shabani, Sunday Mwanahewa na Bakari
Mapande.
Comments
Post a Comment