ECO BANK YADHAMINI 'TOTO PARTY' MAALUM KWA KRISMASMkurugenzi wa Glitz Entertainment Dennis Busulwa 'Ssebo' akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na Toto Party maalum itakayofanyika Desemba 25 na 26 katika ufukwe wa Cine Club Mikocheni, kulia ni mratibu wa maendeleo ya biashara kanda ya Tanzania ya beki hiyo, Adewuvi Adekunle na kushoto ni mkuu wa masoko na bidhaa, Andrew Lyimo

KATIKA kusherehekea sikukuu ya Krismas, watoto  kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wameandaliwa party maalum ‘Toto Party’ inayotarajiwa kufanyika Desemba 25 na 26 kwenye ufukwe wa Cine Club Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Glitz Entertainment iliyoandaa tukio hilo, Denis Busulwa 'Ssebo',amesema kwamba lengo ni kuwakutanisha pamoja watoto hao ili kusherekea sikukuu hiyo sambamba na kupata burudani za aina mbalimbali. 
Alisema watoto watakaohudhuria tukio hilo watapata kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo soka, kuogelea, kuruka, huku pia wazazi wao nao watashindana katika michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba. 
Aliongeza kuwa katika siku hizo kutakuwa na fursa ya ufunguaji wa akaunti maalum kwa watoto kutoka benki ya Eco Bank kupitia akaunti maalum ya watoto iitwayo ‘Pambazuka’ ambapo kila mtoto atakayefungua akaunti hiyo ataingizwa katika bahati nasibu maalum. 
“Akaunti hii ni muhimu kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka 18 ambapo fedha zake ni mahususi kwa ajili ya kuwasaidia katika elimu, hivyo tunaomba wazazi kujitokeza kwa wingi na pia kila anayehitaji kumfungulia mtoto wake gharama ni sh 10,000,”alisema