KATIKA kusherehekea sikukuu ya Krismas, Club yenye hadhi ya
kimataifa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Bilicanas, kesho inatarajiwa
kuwapa burudani kabambe mashabiki wa muziki wa disko wakiwemo watoto.
Mmoja ya viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omary alisema amesema leo kwamba
kwamba, kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo ndiyo maana wameandaa burudani
kabambe ili kutoa fursa kwa watu wa rika lote kusherehekea kwa furaha.
Alisema shamrashamra hizo zitaanza usiku wa leo ambapo kutakuwa na
usiku wa Kwaito ‘Kwaito Special’ uliongozwa na kundi la Wakali Dancers.
Omary alisema, kesho (jumanne) mchana kutakuwa na Watoto Shoo ambapo
pamoja na muziki wa disko watoto watakaojitokeza ukumbini hapo wataburudika na
Father Krismas ambaye atamwaga zawadi ambapo kiingilio kitakuwa sh 2,000 kwa
kila motto huku wakubwa watakaoambatana nao watalipa sh 3,000.
“Usiku wa Krismasi utakuwa na shamrashamra nyingi ambapo
watakaongia kila mmoja atapata mvinyo mwekundu au mweupe, hii kiingilio
kitakuwa sh 10,000 kwa kila mmmoja,”alisema.
Aidha, Omary aliongeza kwamba siku ya boxing Day ukumbi huo
utaendelea kupambwa na burudani mbalimbali ambapo kiingilio kitakuwa sh 5,000
kwa kila mmoja.
Comments
Post a Comment