ABDALLAH JUMA WA SIMBA AWANIWA NA TIMU TANO


PAMOJA na kutong’ara kwenye timu yake katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom, mshambuliaji wa Simba Abdallah Juma ameonekana lulu kwa timu nyingine baada ya kuwaniwa na timu zaidi ya tano. 
Nyota huyo ambaye alisajiliwa na Simba mawaka jana akitokea kwa maafande wa JKT Ruvu, aliweza kung’ara zaidi na timu hiyo kwenye mechi za kirafiki wakati wa maandalizi wa ligi hiyo. 
Habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinaekleza kwamba tayari vilabu vya Pamba ya Mwanza, Coastal Union ya Tanga, Tanzania Prisons ya Mbeya, African Lyon na Ruvu Shooting. 
Kiongozi mmoja wa Simba alisema hivi karibuni kwamba, timu hizo zimetuma maombi ya kutaka kumsajili kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo pamoja na ligi daraja la kwanza, lakini mpka sasa bado hawajaamua juu ya suala hilo. 
“Ndiyo hivyo bado hajuaamua juu ya suala la Abdallah kwanmi hata sisi pia ni mchezaji muhimu kwetu…tunasubiri majadiliano ya kamati ya ufundi kwanza ndipo tutakapotoa maamuzi na pia dau nono litazingatiwa,”alisema. 
Aidha, kiongozi huyo aliongeza kuwa nyota wao Haruna Shamte pia ameomba na klabu ya African Lyon  ambapo viongozi wa pande zote wapo kwenye mazungumzo.