SHIRIKISHO la soka Tanzania
(TFF) linaamini kutumika kwa tiketi za kielektroniki katika mechi mbalimbali
nchini utakuwa ni muarobaini wa tatizo la mapato.
Benki ya CRDB ndiyo imepewa
tenda ya kutayarisha tiketi hizo ambazo zitaanza kutunmika rasmi katika
mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom mwezi Februari mwakani.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Rais wa TFF Leodger Tenga alisema kwamba hatua hiyo ni jambo la
heri na muhimu sana katika kipindi hiki ambacho wadau wamekuwa wakilalamikia
suala la upatikanaji wa mapato kiduchu.
Alisema pamoja na uzuri wa
jambo hilo, lakini wengi watashtuka na kutaka kurudisha nyuma mchakato huo
utakaojenga heshima, lakini Shirikisho hilo halitakubali kurudishwa nyuma.
“Najua wengi litawaathiri
sana kwa namna moja ama nyingine na hivyo kuanza kuleta vikwazo ili
lisifanikiwe, tumesimama imara kuhakikisha hili linatimia ili kujenga
heshima,”alisema Tenga
Comments
Post a Comment