TFF YATUA ENGLAND KUMSAKA ADAM NDITI


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) lipo katika mchakato wa kutaka kukutana na uongozi wa Shirikisho la soka England (FA) ili kuweza kupata mwongozo wa jinsi ya kumpata nyota wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya Chelsea ya huko, Adam Nditi (pichani). 
 Katibu Mkuu wa TFFAngetile Osiah ameiambiaSports Lady  leo kwamba lisema jana kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya awali kugonga mwamba ya kumpata mchezaji huyo kwa ajili ya kumtumia katika timu ya taifa ya vijana. 
Alisema alisema tayari wameshawasiliana na mmoja ya maofisa ubalozi huo, Amos Msanjila ili aweze kuwawekea maziungira mazuri ya kukutana  na FA kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo. 
“Mwanzo tulipogonga mwamba kumpata mchezaji huyu mdipo tuliposhauriwa kuongea na ubalozi wetu ili wao wazungumze kwanza na FA na kutuandalia mazingira ya kukutana nao na kuanza mchakato wa kumuomba Nditi,”alisema 
Osiah aliongeza kuwa anaamini zoezi hilo litafanmikiwa na hivyo nyota huyo ataweza kuja kuyichezea timu ya Taifa ‘Taifa Stars’  katika mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.