MBUYU TWITE AFUNGIWA MAISHA

SHIRIKISHO la soka nchini Rwanda (FERWAFA) kimemfungia maisha kuichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo 'Amavubi' beki  kati wa Yanga, Mbuyu Twite (pichani), imefahamika.
Hatua hiyo inafuati beki huyo anayetambulika kama Eric Gasana kwenye kikosi cha Amavubi kuonyesha utovu wa nidhamu kwa uongozi wa shirikisho hilo baada ya kugoma kujiunga na timu ya Taifa.
Habari zinaeleza kwamba, Twite aligoma kujiunga na timu hiyo inayoshiriki michuano ya Chalenji kwa madai kuwa anahitaji kupumzika baada ya kuitumikia timu yake ya Yanga kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara.