MASHINADNO YA GOFU YA JOHNIE WALKER KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO

Kampuni  ya  Precision Air kwa kushirikiana na kampuni ya bia ya Serengeti, na SBC (Pepsi) T Limited  wamedhamini mashindano ya gofu ya Johnnie Walker Waitara yatakayo fanyika mwisho wa wiki hii.
Mashindano haya maarufu kama  Johnnie Walker  Waitara  Trophy  yatafanyika kuanzia ijumaa na jumamosi wiki hii katika viwanja vya gofu vya Lugalo.
Mashindano hayo yatashirikisha wachezaji 120 watakaoshindania kikombe na fedha taslimu huku washindi wengine watano wakijishindia tiketi tano za ndege kutoka Presicion Air.

Akizungumza wakati wa kuzindua michuano hiyo, Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,  Emilian Rwejuna,  amesema  kampuni hiyo imekuwa mdhamini mkubwa wa mashindano hayo kila mwaka.
“Tunathamini mchezo wa gofu nchini na wachezaji kwa ujumla na ndio maana  tumeamua kujikita katika mchezo huu. Mbali na kudhamini mchezo wa gofu. Johnnie Walker    imekuwa ikijihusisha na michezo mingine kama mashindano maarufu ya langalanga kupitia timu ya  Mclaren  Mercedes yenye wachezaji kama  Lewis Hamilton na Jenson Button, na pia Johnnie Walker imekuwa ikijihusisha na watu maarufu katika michezo na sanaa zingine kama  wanariadha maarufu  Gabriel Haile selasie,
Manu Dibango na wengine wengi. Johnner Walker ina kauli mbiu yake ya KEEP WALKING.

Mratibu wa masoko wa kampuni ya  Precision Air,  Hillary Mremi    amesema kuwa kampuni yao iko katika msitari wa mbele  kukuza vipaji na michezo nchini.
“Tumejipanga vyema kuhakikisha tunachangia maendeleo ya michezo nchini, kwani wanamichezo wetu ndio mabalozi wazuri kwa nchi yetu hivyo ni jukumu letu kuwasaidia wao kufanya vizuri,” alisema  Mremi.
Tunajisikia fahari kuwa sehemu ya mashindano haya, kwani itakuwa ndiyo njia pekee ya kukuza mchezo nchini.”

Wengine waliokuwa katika uzinduzi ho ni pamoja na Foti Gwebe Nyirende, Mkuu wa huduma za jamii wa SBC, watengenezaji wa kinywaji cha pepsi ambao pia ni wadhamini wa mashindano hayo.