MAKOCHA ZANZIBAR KUANZA KUNOLEWA KESHO


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) linatarajiwa kuendesha kocha maalum kwa makocha wa leseni C na waandamizi inayotarajiwa kuanza kesho hadi Desemba 10 katika Uwanja wa Amaan,  Visiwani Zanzibar. 
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameiambia Sports Lady  kwamba wameamua kuendesha kozi hiyo ili kuondoa dhana iliyojengeka ya kwamba wamekuwa wakiwatenga Wazanzibar katika mambo mbalimbali. 
Alisema kozi hiyo itaendeshwa na mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho hilo, Sunday Kayuni akishirikiana na mjumbe wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmed Babekir kutoka Sudan. 
Alisema baada ya kumalizika kocha kwa makocha wa daraja hilo, itafuata ya makocha waandamizi itakayoanza Desemba 11 hadi 14 katika uwanja huo. 
Alisema mara baada ya kufanyika kwa kozi hiyo makocha waandamizi watafanyiwa tathimini na kupatiowa vyeti maalum vya daraja B vinavyotambuliwa na CAF .