YANGA WAHAMISHA KAMBI ILI KUJIWEKA SAWA NA MECHI YAO NA SIMBA KESHO


ZIKIWA zimeabaki saa kadhaa kabla ya pambano la watani wa jadi nchini Simba na Yanga, kikosi cha Yanga kimehamisha kambi yake kutoka hoteli ya Up lands iliyoipo Changanyikeni jijini Dar es Salaam hadi hoteli yenye nyota tano, Double Tree By Hilton, imefahamika.

Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako amesema kwamba wameamua kuhamisha kambi hiyo ili kuwaweka wachezaji katika mazingira mazuri zaidi ya kimchezo.

Alisema kikosi hicho ambacho kipo katika hali nzuri, kiliingia katika hoteli hiyo juzi baada ya mchezo wao wa ligi dhidi ya African Lyon, kinafanya mazoezi yake katika viwanja vya Sekondari ya Loyola.