SIMBA YAPIGA MKWARA MZITO TFF KUHUSU FEDHA ZA TWITE


MABINGWA wa ligi kuu bara Simba wamesema watatoa tamko la kuushangaza umma wa Watanzania iwapo klabu ya Yanga haitawarejeshea dola 32,000 walizompatia  wa beki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mbuyu Twite kwa ajili ya kujisajili. 
Twite ambaye alikuwa akiichezea APR ya Rwanda awali Simba ilimsainisha mkataba wa kuichezea katika msimu huu, kabla ya Yanga kuingilia na kumsajili kwa dau la dola 50,000. 
Kutokana na kitendo hicho, Simba ilishitaki kwa kamati ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji  ya TFF ambayo ilitoa maamuzi ya Septemba 10 na kuitaka Yanga irejeshe fedha hizo ndani ya siku 21 ambazo zilimalizika jana.
 Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba wanailaumu TFF kwa kutoitendea haki kuhusiana na suala hilo. 
“Hiyo ni baada ya kimya kingi tuliandika barua TFF ili kukumbushia juu ya suala hilo, lakini kuna kiongozi mmoja alitujibu kwa mdomo kuwa tuandike wenyewe barua Yanga kukumbushia malipo hayo kitu ambacho hakileti mashiko kabisa,”alisema 
Aliongeza kuwa kwa suala hilo wamekaa kimya la kwa Okwi kufungiwa mechi tatu na kulipa faini  walituletea barua haraka bila ya bila kuomba. 
Hata hivyo, Yanga kupitia kwa Katibu wake, Lawrance Mwalusako alisema kwamba suala hilo lipo katika mpangilio mzuri na kama Twite akicheza kesho dhidi ya Simba  ujue wamemalizana na Simba.

Comments