MISS TANZANIA JACQUELINE NTUYABALIWE AJIFUNGUA MAPACHA
MISS Tanzania 2000 Jacquiline Ntuyabaliwe amefanikiwa kujifungua salama watoto mapacha wa kiume.
Habari zilizopatikana jijini zinaeleza kwamba mrembo huyo pamona na watoto wake hao hali zao zinaendelea vema.
Pamoja na urembo, Jacquiline pia amekuwa akijihusisha masuala ya muziki wa bongo fleva akijulikana kama K'Lyn  ambapo aliwahi kutoa nyimbo kadhaa zilizoweza kufanya vema katika medani hiyo kabla ya kuachana nao na kuamua kuwa mjasiriamali.
Sports Lady Blog inampongeza K_lyn kwa kuingia katika ulimwengu wa wazazi na tunakutakia afya njema na malezi mema ya watoto wako wapya.