KIBALI CHAMFANYA KOCHA MPYA YANGA AWAKOSE SIMBA


Brandts
KOCHA  mpya wa Yanga Ernstus  Brandts anashindwa  kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kutokana na  kutokuwa na kibali cha kazi.
Brandts aliyejiunga na Yanga jumamosi iliyopita atashindwa kuongoza benchi la timu hiyo keshokutwa itakapokwaana na  mahasimu wao Simba, katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako amesema  kutokana na kukosa kibali hicho Brandts  ataendelea kutoa ushauri tu wa kiufundi kwa benchi la timu hiyo mpaka pale atakapopata kibali cha kuifanya kazi nchini na hivyo  kwa sasa kocha msaidizi Fred Felix Minziro ataendelea kukalia benchi hilo.
 “Mpaka sasa kocha hajapata kibli cha kufanya kazi hivyo anachofanya ni kutoa ushauri tu wa kiufundi…lakini tunatrajia siku mbili hizi kitapatikana na hivyo atakabidhiwa rasmi mikoba yake,”alisema.