MISS KINONDONI 2012 KUZAWADIWA SITTING ROOM SETMratibu wa shindano la Miss kinondoni 2012 Vivian Sirikwa kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, kulia ni meneja wa bia ya Redd's Victoria Kimaro.
WAKATI shindano la kumsaka Redd’s Miss Kinondoni  2012 likipangwa kufanyika Septemba 14, mrembo atakayetwaa taji hilo atazawadiwa Seti ya vifaa vya sebuleni ‘Sitting Room Set’ vyenye thamani y ash milioni tano.
Shindano hilo litafanyika  kwenye ukumbi wa Cassa Complex uliopo Mikocheni, ambapo warembo 10 watachuana kuwania taji hilo linaloshikiliwa na Stela Mbuge.
Mratibu wa shindano hilo, Vivian Sirikwa alisema kwamba maandalizi yanakwenda vema ambapo warembo hao walitarajiwa kuingia kambini jana kwenye hoteli ya JB Belmonte iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Alisema mwaka huu wamedhamiria kurejesha heshima ya Kanda hiyo kwa kuhakikisha wanatoa warembo bomba ambao mmojawapo ataweza kutwaa taji la Miss Tanzania mwaka huu.
“Kama mnavyoona warembo wetu wa mwaka huu walivyo bomba,hii ni mikakati yetu ya kutaka kurejesha hadhi ya Kino0ndoni katika mashindano ya urembo…tunapenda kuwahakikishia wadau wa urembo kwamba mwaka huu Kinondoni itaandika historia,”alisema
Mratibu huyo aliongeza kwamba, kabla ya kufanyika kwa shindano hilo, Jumatano ya Septemba 12 kutafanyika shindano la kusaka vipaji ‘Talent Show’ kwenye ukumbi wa Savanna Lounge uliopo jengo la Benjamin Mkapa Tower, huku pia wakitaraji kumsaka balozi wa hospitali ya Mwananyamala ambapo mshindi atakuwa akifanya kazi za kijamii katika hospitali hiyo kwa mwaka mzima.
Mbali na zawadi hiyo kwa mshindi wa Kwanza, mshindi wa pili atapata Jokofu la size ya familia lenye thamani y ash milioni tatu, huku mshindi wa tatu atapata tv bapa ya inchi 32 yenye tahamani y ash milioni 1.5, wakati mshindi wanne atapata sh 500,000, mshindi wa tano ataondoka n ash 300, 000 na washiriki waliosalia kila mmoja atapata sh 100,000.
Aliwataja warembo watakaowania taji hilo kuwa ni pamoja na Diana Hussein, Kudra Lupatu, Esther Musa, Brigitte Alfred, Jennifer Manu, Judith Sangu, Zulfa Vuai, Mahma Said, Mwantumu Mustafa na Irene David.
Shindano hilo ambalo limeandaliwa na kampuni ya Up and About limedhaminiwa na Redd’s Oroginal, JB Belmonte Hotel, Brilliant Mens Boutique, Skylight Entertainment, Kas Freight Limited, Clouds Fm, Magic Fm na Channe 10.