KLABU KUTETEA PINGAMIZI ZA WACHEZAJI


Klabu zote zilizowekewa pingamizi za wachezaji kwenye usajili na zile zilizoweka pingamizi zinatakiwa kufika kwenye kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitakachofanyika kesho (Septemba 4 mwaka huu).

Kikao hicho kitafanyika kwenye ofisi za TFF kuanzia saa 6 kamili mchana, na kitakuwa chini ya uenyekiti wa Alex Mgongolwa.

Klabu ambazo zimewekewa/ kuweka pingamizi na zitakiwa kuwepo kwenye kikao zilikiwa na nyaraka zote kuthibitisha madai yao ni Azam, African Lyon, Flamingo, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Oljoro JKT, Polisi Mara, Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation, Simba, Super Falcon, Toto Africans, Villa Squad na Yanga.