ZIARA YA AFC LEOPARDS YAOTA MBAWA


ZIARA ya timu  AFC Leopards ya Kenya iliyokuwa itue nchini imeota mbawa. 
Leopards inayoshiri Ligi kuu ya Kenya ilikuwa icheze na vigogo vya soka nchini Simba na Yanga ambapo leo ilitarajiwa kucheza na Simba katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. 
Mmoja ya waratibu wa ziara hiyo George Wakuganda alisema wameamua kufuta ziara hiyo kutokana na kukosekana kwa viwanja. 
Alisema wamiliki wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid wameshindwa kuruhusu kutumika uwanja huo kwa ajili ya mechi kutokana na kuwa katika matengenezo. 
Aliongeza kuwa, hata mchezo baina ya Leopard na Yanga ambao ulipangwa kuchezwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam nao hautakuwepo kwa sababu ya kukosekana kwa uwanja.