YANGA V LYON SASA J'3 TAIFA, YANGA V COASTAL UNION WAFUTWA


MCHEZO wa kirafiki kati ya Yanga na African Lyon,utafanyika Jumatatu
kwenye uwanja wa Taifa ,Dar es Salaam badala ya Jumapili.

 Katibu Mkuu wa Yanga,Mwesigwa Celestine alisema kuwa hatua hiyo imefikia baada ya
wammiliki wa uwanja huo kutoa nafasi kwa siku hiyo.

Awali mchezo huo,ulikuwa ufanyike siku ya Jumapili na Jumatatu ambapo
Yanga ilitarajiwa kucheza na timu ya Coastal Union ambao umefutwa
kutokana na tatizo hilo la uwanja.

Akizungumzia mchezo huo,Mwesigwa ameeleza kwamba kikosi chao kinaendelea na mazoezi ya nguvu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola ambapo nyota karibu  wote wapo.

Aliongeza kuwa kwenye mchezo huo,watawachezesha wachezaji wao wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao  ambapo ligi kuu ya bara inatarajiwa kuanza Septemba Mosi.
Miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kuwemo katika mchezo huo ni Didier Kavumbagu,Mbuyu Twite,Frank Domayo na wengine ambao bado hawajaichezea timu hiyo hata mechi moja.

Kwa upande wa mmiliki wa timu ya African Lyon,Rahim 
Kangezi ametamba kwamba kikosi chake kipo imara na kitaifundisha soka timu ya Yanga
katika mchezo  huo huku akitamba kuwatumia nyota wao watatu kutoka nje ya nchi.
Alisema kwamba baada ya kuanza mazoezi ya nguvu,wapo tayari kwa ajili ya kupambana na Yanga siku hiyo ambapo wamepania kufanya kweli huku wakipanga kuwatumia baadhi ya nyota waliowasajili.


Ametamba kuwa wao wamefanikiwa zaidi baada ya kuwasajili wachezaji wengi kinda ambao ana uhakika wataweza kufanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya Yanga.


Mmiliki huyo amevitaja viingilio kwenye mchezo huo ni shilingi 15,000 VIP A wakati VIP B ni shilingi 10,000 huku upande wa viti vya rangi ya machungwa ni shilingi 5,000 na mzunguko shilingi 3,000 na kuwataka mashabiki wa soka kufika kwa wingi ili kuona jinsi kikosi chao

kitakachotoa dozi kwa Yanga.

Comments

Post a Comment