TWITE ATUA, AVIKWA JEZI NAMBA 4 YENYE JINA LA RAGE

 Beki wa kimataifa wa Yanga Mbuyu Twite akionesha jezi namba 4 aliyovikwa na mashabiki wa Yanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege leo. Jezi hiyo ambayo imeandikwa 'RAGE' ni jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage inanokana ni kijembe kwa mahasimu hao wa Yanga ambao awali walitangaza kumsajili kwa dau la dola 30,000 kabla ya Yanga kumpandishia hadi dola 50,000.
 Hapa Twite akivishwa jezi hiyo yenye jina la Rage na mwanachama maarufu wa Yanga

 Twite akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema amekuja kufanya kazi na hajali yote yaliyosemwa juu yake kujisajili timu mbili
 Hapa Twite akiingia kupitia mlango wa watu mashuhuri (VIP) uwanjani hapo akiambatana na baadhi ya viongozi wa Yanga
 Watu TWITE TWITE TWITEEEEEEEEEE 
 Kulikuwa na mbwembwe za kila aina na uwan ja ulifurika kwa rangi zxa njano na kijani
 Matarumbeta , mdundiko vilikuwepo yote ni katika furaha ya ujio wa Twite
Kwa mapenzi na timu yao hawakujali kama ni muda wa kazi, jua, mvua wala kupoteza muda ,kwao ilikuwa ni full  shangwe na hatimaye FILAMU Ya TWITE ILIISHA.