SIMBA SASA KUIVAA MATHARE UNITED J'2, SUNZU YU MGONJWA

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba, keshokutwa watacheza mechi ya kimtaifa ya kirafiki dhidhi ya Mathare United ya Kenya, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Awali Simba ilikuwa icheze na AFC Leopard ya Kenya siku ya Jumapili lakini kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika imebidi wabadili timu ya kucheza nayo.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwamba maandalizi kwa ajili ya mchezo huo na kwamba wachezaji wote wapo katika hali nzuri isipokuwa mshambuliaji wao wa kimtaifa Mkenya Felix Sunzu ambaye anasumbuliwa na Malaria.