EMMANUEL OKWI KUTUA DAR LEO


WAKATI mshambuliaji anayewapagawisha Simba, Mganda Emmanuel Okwi, akitarajiwa kutua nchini leo, klabu hiyo kesho imepanga kutambulisha nyota wake wapya katika Tamasha la Simba Day.
Katika tamasha hilo, Simba itakwaana na City Stars ya Kenya katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, alisema Okwi atawasili nchini akitokea kwao Uganda.
Nyota huyo anakuja nchini wakati akisubiri majibu yake ya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu ya Red Bull Salzburg ya nchini Austria.
Alisema, Okwi pia atashiriki katika mechi hiyo dhidi ya City Star, ambayo ni maalum sambamba na mshambuliaji wao mpya waliyemsajili kutoka Azam FC, Mrisho Ngasa na wengineo.