AFC LEOPARDS KUTUA KESHO TAYARI KUZIVAA, YANGA NA SIMBA


TIMU ya FC Leopards ya Kenya inawasili nchini kesho tayari kwa kuwavaa Simba na Yanga, katika mechi za kirafiki za kirafiki za kimataifa kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba ndio watakaonza kucheza keshokutwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, na Yanga watacheza Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Akizungumzia ujio wa timu hiyo, Mratibu wa mechi
hiyo, Kennedy Mwaisabula alisema kila kitu
kinakwenda vizuri na wanatarajia mechi hizo
zitajaa upinzani mkali kutokana na jinsi timu
hiyo ilivyo.
"FC Leopards ni timu nzuri kila mmoja anaijua
kwani inaupinzani mkali sana katika Ligi Kuu ya
Kenya, na ndio maana tukaiomba ije kwa ajili ya
kuzinoa timu zetu," alisema Mwaisabula.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Simba Milovan
Cirkovic alisema mechi hiyo itakuwa kipimo kizuri
kwa wachezaji wake wapya kwani ataweza kubaini
mapungufu katika kikosi chake.
"Ni mechi nzuri ambayo naimani kabisa
itaniwezesha kujua mapungufu katika kikosi
changu, hivyo nawataka wachezaji wangu waitumie
vizuri kwani ninafasi nyingine kwao katika
kutafuta namba katika kikosi cha kwanza," alisema
Milovan.
Alisema wakicheza mechi hiyo atatafuta mechi
nyingine zaidi ili aweze kukipika vizuri kikosi
chake, kwani katika michuano ya Kombe la  Kagame
aligundua mapungufu mengi.

Comments