NITATATUNDIKIA DALUGA CHINA-ANELKA


MSHAMBULIAJI wa zamani wa  Chelsea  Nicolas Anelka amevunja ukimya kuhusiana na uvumi ulioenezwa kwamba ana mpango wa kurejea  England na kusema kwamba atatundika daruga akiwa katika klabu yake ya sasa ya Shanghai Shenhua ya China. 
Hivi karibuni kulikuwepo na taarifa kwamba nyota huyo mwenye miaka 33 amekuwa akiwaniwa na klabu zinazoshiriki ligi kuu ya England QPR  na  West Ham. 
Anelka  alisaini mkataba wa miaka miwili na  Shenhua mwezi Desemba mwaka 2011, ambapo kwa sasa timu hiyo  inashika nafasi ya 13 katika ligi kuu ya China.