NI YANGA AU AZAM KUBEBA MWALI WA KAGAME LEO


MABINGWA watetezi wa kombe la KAgame Yanga SC, pamoja na mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC leo wanashuka katika dimba la Taifa katika mchezo wa fainali ya kombe la Kagame.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kiasi cha kuwafanya mashabiki wa soka nchini kushindwa kubashiri ni timu ipi itanyakua ubingwa huo.
Wakati Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kuifunga APR ya Rwanda, Azam inayoshiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza ilikata tiketi ya fainali baada ya kuitoa Vita Club ya JAmhuri ya KIdemokrasia ya Congo.
Tayari makocha wa pande zote Stewart Hall (Azam FC) na Tom Saintfiet wa Yanga kila mmoja ametamba timu yake kuibuka na ushindi kutokana na kuzipa maandalizi kabambe.
Hata hivyo kila mmoja amedai kukiheshimu kikosi cha mwenzie na kusema kipyenga cha mwisho ndicho kitaamua nani atacheka nani atanuna.