MASHUJAA MUSICA KUTAMBULISHA WAPYA WAKE DOM IJUMAA


BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa ‘Wana Kibega' keshokutwa wanatarajiwa kufanya  onesho maalum la kutambulisha wanamuziki wao wapya kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma kupitia onyesho litakalofanyika ukumbi wa Royal hotel mjini humo. 
Meneja Mashujaa Martin Sospeter, alisema kuwa  wameamua kufanya hivyo ili kuwapa fursa mashabiki wao kuwashuhudia ‘live’ wanamuziki hao wapya ambao wameongeza nguvu katika bendi hiyo ambayo kwa sasa ni moja ya bendi pendwa. 
Alisema pamoja na utambulisho huo, onesho hilo pia litaambatana na utambulisho wa nyimbo mpya zilizotungwa hivi karibuni na nyingine ambazo zimeanza kufanya vema katika vituo mbalimbali vya redio. 
“Kama mjuavyo tuna wasanii wapya kama kina Charlz Baba, baba Diana, Ferguson, MCD, 33, Lilian Internet na wengineo ambao tangu wajiunge na bendi yetui hatujawatambulisha katiuka baadhi ya miji hivyo sasa hivi ni fursa kwa wakazi wa mji wa Dodoma,”alisema. 
Aidha, meneja huyo alisema kuwa bendi hiyo leo  itakuwa na onesho lake maalum kwa wakazi wa Yombo kwa Jimmy baada ya hapo itaanza safari ya kwenda Dodoma, kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam kuendelea na ratiba zao nyingine ikiwemo bonanza lao la kila Jumapili kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe.