MASHABIKI WA SIMBA WAENDELEA KUJISHINDIA BAJAJ, PIKIPIKI




Afisa habari wa mabingwa wa soka wa Tanzania, Simba SC, Ezekiel Kamwaga (kulia) akimkabidhi  ufunguo mpenzi wa timu hiyo Abubakari Hamis (katikati) kutoka Arusha baada ya kuibuka mshindi katika bahati nafasi ya Simba Fan Club katika hafla fupi  jana. Kushoto ni meneja wa kampeni hiyo, Talib Rashid kutoka kampuni ya Push Media Moobile. Washiriki wa bahati nasibu hiyo wanatakiwa kutuma neno Simba kwenda kwenye namba “15678” na kuingia katika droo.

Na Mwandishi wetu
KLABU ya Simba imewataka wapenzi na mashabiki wake kuendelea kujiunga na huduma ya kutuma ujumbe mfupi kupitia huduma ya Fan Simba Club ili kupata taarifa mbalimbali za Simba ikiwemo matokeo ya michuano ya kombe la Kagame  inayoanza Julai 14 mwaka huu na masuala ya Usajili.
Akizungumza Dar es Salaam , Ofisa Habari wa Klabu hiyo Ezekiel Kamwaga alisema kupitia huduma hiyo mashabiki wa Simba watapokea taarifa  za kila siku  ambazo wao watakuwa wa kwanza kuzipata kupitia huduma hiyo.
Alisema pia itaisaidia klabu ya Simba kujiongezea mapato yatakayoiwezesha klabu hiyo kuendesha mambo yake katika ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri.
Kwa upande wake Meneja  Kampeni wa Kampuni ya Push Mobile Talib Rashid ambao wameingia mkataba na klabu ya Simba kupitia huduma ya sms Fan Simba Club wamefunga droo ya bahati nasibu waliokuwa wakiichezesha kwa klabu ya Simba kupitia huduma hiyo kwa kutoa pikipiki na bajaji.
Bahati nasibu hiyo iliyokuwa ikichezwa kwa kipindi cha miezi mitatu sasa imefungwa kwa kuwapata washindi ambao ni wanafunzi wa shule za Sekondari huku mmoja akiwa ni Tito Zakaria kutoka shule ya Sekondari ya Mong'ola iliyopo Dodoma aliyejishindia pikipiki na Mohamed Ibrahim kutoka shule ya Sekondari ya Chandama iliyopo Kondoa na kujishindia bajaji.

Comments