KUWAONA YANGA NA JKT KESHO SH.3,000


Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu kushoto pamoja na mratibu wa mechi baina ya Yanga na JKT Ruvu Salum Mkemi wakizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mechi hiyo itakayopigwa kesho katika Uwanja wa Taifa ambapo kiingilio cha chini kitakuwa shilingi 3,000 kwa mashabiki watakaokaa viti vya kijani na Bluu.
 “Kwa mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya chungwa watalipa sh.5000, huku watakaokaa VIP B na C watalipa shilingi 10,000 na watakaokaa VIP A watalipa sh.15,000,”alisema Mkemi.