KOCHA MPYA YANGA KUANZA KAZI KESHO

KOCHA mpya wa Yanga Mbelgiji Tom Saintfe anatarajiwa kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho jioni ya kesho mara baada ya kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema leo kwamba tayari uongozi umeshazungumza na kocha huyo juu ya majukumu yake.
Yanga inaendelea na maandalizi yake ya michuano ya Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 15 jijini Dar es Salaam kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi, Fred Felix Minziro.