KAMATI YA UCHAGUZI YANGA YAONYA WANAOFANYA KAMPENI CHAFU


Francis Kaswahili 


Kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo imetoa hadhari juu ya uwepo wa kampeni chafu. 
Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili amesema  kwamba kuna baadhi ya wanachama wamekuwa wakipitisha karatasi yenye nembo ya Yanga ikiwatambuylisha baadhi ya wagombea kuwa ndio wameteuliwa kuongoza klabu hiyo. 
Alisema kufanya hivyo ni kuingilia misingi na haki za wagombea wengine hivyo watakaobainika atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kuongeza kuwa Kamati ya uchaguzi ya Yanga ndiyo ina mamlaka ya kumtangaza mshindi. 
Aidha, Kaswahili alitoa onyo kwa baadhi ya wanachama kutishia kwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi na kusema kuwa atakayefanya hivyo atashitakiwa kwa kamati ya nidhamu ya Yanga kabla ya kufutwa uanachama.