GEORGE MANYAMA :ANAYETAKA KUINGIA YANGA ILI IACHANE NA UMATONYA


Manyama anasema ameamua kujitosa kuwania nafasi hiyo kwa lengo la kuifanya Yanga ijitegemee na kuondokana na hali ya kusubiri ufadhili.
Anasema iwapo atafanikiwa kutwaa nafasi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake atahakikisha wanaifanya Yanga inakuwa tishio ndani na nje ya nchi kwa kushinda mataji mbalimbali.
Manyama ambaye ni mfanyabiasha, anasema aanauzoefu wa kuongoza kwani kwa miaka 15 amekuwa akiisaidia Yanga kwa namna moja ama nyingine.
“Mimi kama mfadhili wa tawi la Yanga Kigogo nadhani ni wakati wangu wa kuleta utaalamu wangu wa kuongoza katika Yanga yetu...naombeni kura zenu.