FID Q AFUNIKA SHOO YA WAJANJA MTWARA


Katika hali isiyotarajiwa na wengi Msanii na Mkali wa Bongo Fleva Farid Kubanda maarufu kama Fid Q juzi alifunika katika shoo wa Wajanja tour  ya Vodacom iliyofanyika Mtwara jumapili hii na kusababisha mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo kukataa asishuke jukwaani.
Fid Q aliepanda jukwaani majira ya saa kumi na moja na nusu baada ya Diamond kumaliza Shoo yake,  na alipopanda jukwaani umati wa wana Mtwara ulilipuka kwa shangwe na kuwapa wakati mgumu mabaunsa waliokuwa wakisimamia shoo hiyo. Hata alipomaliza nyimbo zake mashabiki walipiga kelele kutaka aendelee kuimba na kumwita Ngosha! Ngosha!Ngosha!nakuanza kulisukuma basi alilo[panda msanii huyo mpaka nje ya uwanja.
Wasanii wengine waliofunika katika Show hiyo ni Pamoja na Diamond, Shetaa, Ney wa mitego na Mabeste,

Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kuwa Tour ya Wajanja wa Vodacom itafanyika siku ya jumapili ya wiki hii Mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.

"Wajanja tour sasa inaelekea kwa "waja leo waondoka leo" mkoani Tanga baada ya kufunika vilivyo Mkoani Mtwara hivyo wakazi wa Tanga wajiandae kupata burudani kutoka kwa wasanii kibao watakao kuwa katika Tamasha hilo." Alisema Nkurlu.