CHEKA ATAKIWA KULIPA MIL.100 KWA KUINGIA MITINI

SIKU moja baada ya kamisheni ya masumbwi ya kulipwa nchini (TPBO) kumuondoa bondia Francis Cheka katika mabondia wanaowasiamia, promota wa ngumi nchini Kaike Siraju amemtaka bondia huyo kumlipa sh.mil.100.
Hatua hiyo inafuatia Cheka kuingia mitini katika pambano lake la kuwania ngao ya hisani dhidi ya Japheti Kaseba lilokuwa lifanyike Julai 7 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kaike alisema kuwa Cheka hana budi kulipa fedha hizo kama fidia ya ghara zilizotumika katika maandalizi ya mpambano huo.